Hapana. Ikiwa idara ya usalama wa sheria itaanza kuonyesha nia ya kufuatilia usafirishaji wa data kutoka kwenye kifaa chako cha kupeleka mtandao (exit relay), ni sawa kabisa kama maafisa wanaweza kukamata kompyuta yako. Kwa sababu hiyo, njia bora si kutumia exit ralay nyumbani kwako au kutumia mtandao wako wa nyumbani.

Badala yake, fikiria kuendesha exit relay yako ya kutokea katika kituo cha biashara ambacho kinaiunga mkono Tor. Kuwa na anwani ya IP tofauti kwa ajili ya kifaa chako cha kutoa mtandao (exit relay), na usiruhusu usairishaji wa data yako mwenyewe ipite kupitia hiyo. Bila shaka, unapaswa kuepuka kuweka habari yoyote nyeti au binafsi kwenye kompyuta inayohifadhi exit relay yako.