Ikiwa unatumia Debian au Ubuntu hususani, tafadhali tumia hazina ya mradi wa Tor ili uweze kupokea masasisho kwa urahisi. Kwa kuongeza, kutumia kifurushi hutoa manufaa nyingine:

  • ulimit -n yako huwekwa kwa nambari ya juu kwa hivyo Tor inaweza weka wazi miunganisho yote inayohitaji.
  • Kifurushi huunda na kutumia mtumiaji tofauti, kwa hivyo hauitaji kuendesha Tor kama mtumiaji wako mwenyewe.
  • Kifurushi kinajumuisha hati ya init kwa hivyo Tor inaendesha kwenye boot.
  • Tor inaweza kufunga bandari za nambari ya chini, kisha ikashusha vipaumbele.