Vigezo vilivyowekwa katika AccountingMax na BandwidthRate hutumika kwa kazi za watumiaji na utendaji wa relay katika mfumo wa Tor. Kwa hiyo unaweza kugundua kuwa huwezi kuvinjari mara tu Tor yako inapoingia katika hali ya kupumzika, iliyosainiwa na ingizo hili la kumbukumbu:

Bandwidth soft limit reached; commencing hibernation.
No new connections will be accepted

suluhisho ni kuendesha michakato miwili ya Tor - relay moja na mtumiaji mmoja, kila moja kwa usanidi wake. Njia moja ya kufanya hivyo (ikiwa umeanza kutoka katika mpangilio unafanya kazi wa relay) ni kama ifuatavyo:

  • Katika faili la relay Tor torrc, weka tu SocksPort kuwa 0.
  • Tengenza faili jipya la mtumiaji la torrc.chagua na hakikisha inatumia kumbukumbu ya faili tofauti kutoka katika relay. Mkataba mmoja wa kutaja unaweza kuwa torrc.client na torrc.relay.
  • Boresha mtumiaji wa Tor na relay maandishi ya kuanza ikijumuisha -f /path/to/correct/torrc.
  • Katika Linux/BSD/Mac OS X, badilisha maandishi ya kuanza katika Tor.client na Tor.relay inaweza kurahisisha utenganishaji wa usanidi.