Tumedhamiria kuweka mpangilio Tor relay kuwa rahisi na inayowezekana:

  • Ni sawa kama relay wakati mwingine inatoka mtandaoni. Saraka la kutoa taarifa kwa haraka sana itasitisha kuitangaza relay. Jaribu kuhakikisha kuwa haiwi marakwamara, sababu mawasiliano kwa kutumia relay inapokuwa imeacha kujiunganisha yanavunjika.
  • Kila Tor relay inaexit policy ambazo zinabainisha aina gani ya vifaa toka nje vinaruhusiwa kuunganisha au vinakaliwa na relay. Kama haujisikii vizuri kuruhusu watu kutoka katika relay yako, unaweza kupangilia kuruhusu tu mawasiliano katika Tor relay zingine.
  • Relay yako kwa ukimya itakadilia na kutangaza kiwango cha data kilichosafirisha muda mfupi, kwa hiyo relay yenye kiwango kikubwa cha usafirishaji wa data utavutia zaidi watumiaji wengi kuliko yenye kiwango kidogo. Kwahiyo, kuwa na relay yenye uwezo mdogo inafaa pia.