Upo sahihi, kwa sehemu kubwa, Byte kuingia kwenye Tor relay kunamaanisha baytes moja kutoka nje, na vivyo hivyo. Lakini kuna baadhi ya ubaguzi:

Ikiwa umefungua DirPort yako, kisha mtumiaji wa Tor atakuuliza nakala ya saraka. Ombi wanalofanya (HTTP GET) ni dogo sana, na majibu yake muda mwingine ni makubwa sana. Hii inawezekana ndio sababu kubwa ya tofauti kati ya idadi ya bytes"andika" na idadi ya bytes "soma".

Ubaguzi mwingine mdogo huonesha wakati unapofanya kazi kama exit node, na ukasoma baiti chache kutoka muunganiko wa kutoka (Kwa mfano, ujumbe wa papo kwa hapo au mawasiliano ya ssh) na kufunika ndani ya seli nzima ya baiti 512 kwa usafirishaji kupitia mtandao wa Tor.