Tor itarudia kutumia circuit sawa kwa mikondo mipya ya TCP kwa dakika 10, jakokuwa circuit inafanya kazi vizuri. (Kama Circuit zimeshindwa, Tor itahamia kwenye circuit mpya papo hapo.)

Zingatia mkondo mmoja wa TCP (mf. muunganiko mrefu wa IRC) utakaa katika circuit hiyo milele. Hatuzungushi mkondo wa mtu kutoka circuit moja kwenda nyingine. Vinginevyo, adui anaye weza kutazama sehemu ya mtandao anaweza akapata nafasi nyingi kwa muda kukuunganisha na hatima yako, kuliko nafasi moja.