Hakuna ambacho watengenezaji wa Tor wanaweza kufanya kufuatilia watumiaji wa Tor. Ulinzi sawa unaowazuia watu wabaya kujificha kutojulikana katika Tor, pia unatuzuia kuweza kuona kile kinachoendelea.

Baadi ya mashabiki wamependekeza kuwa tutengeneze upya Tor tuhusishe mlango wa dharura] . Kuna matatizo mawili katika hili. Kwanza, inadhohofisha mfuu mbali kabisa. Kuwa na njia kuu ya kuunganisha watumiaji katika kazi zao ni pengo kwa washambuliaji wote; na mbinu za sera inatakiwa kuhakikisha utunzaji sahihi wa majukumu haya sio ya kwaida na hayatatuliki. Pili, watu wabaya hawakamatwi kwa namna hii ] , kwa kwakuwa watatumia njia nyingine kuhakikisha hawatambuliki (utambuzi wa wizi, kujimilikisha kompyuta na kutumia kama alama za ukwepaji, na kadahilika).

Hii humaanisha kuwa ni wajibu wa wamiliki wa tovuti kujilinda dhidi ya mambo ya usalama ambayo yanaweza kutoka popote. Hii ni sehemu ya kujiandikisha kwa manufaa ya mtandao. Unatakiwa ujiandae kujilinda dhidi ya viashiria vibaya, kokote vitakavyotokea. Udukuzi na kuongezeka kwa ufatiliaji sio suluhu ya kuzuia unyanyasaji.

Kumbuka hii haimaanishi kwamba Tor haipatikani. Mbinu za jadi za police bado zinaweza kuwa na athari dhidi ya Tor, kama vile njia za kiuchunguzi, nia, na nafasi, kuhoji watuhumiwa, uchambuzi wa mtindo wa uandishi, uchambuzi wa kiufundi wa maudhui, operesheni danganyifu,kufunga pingu na aina nyingine za uchunguzi. Tor Project inayo furaha kufanya kazi na mtu yeyote wakiwemo vikundi vya watekelezaji wa sheria tuwafundishe namna ya kutumia proggramu ya Tor kufanya uchunguzi kwa usalama au kujojulikana katika shughuli za mtandaoni.