Hapana, Tor Browser ipo kwa ajili hiyo. Tunatambua kwamba mamilioni ya watumiaji ulimwenguni, hujikita katika Tor Browser na masuluhisho mengine ambayo Tor Project hutoa kujiunganisha salama katika mtandao, peruzi online bila kujulikana na ukwepaji wa udhibiti. Hivyo Tor Browser itaendelea kuwepo. Kuna sababu nyingi za kuendelea kudumisha na kuboresha Tor Browser, bado ni moja ya suluhu chache ambayo inatoa kutojulikana mtandaoni kwa sababu ya utumiaji wa mtandao wa Tor. Muunganiko huu ni imara na muda mwingine moja kati ya machaguo ambayo watumiaji waliodhibitiwa na kufuatiliwa katika mikoa yao hupata mtandao bure na salama. Hii pia ni suluhusho la bure kwa wote, imefanya kuwa suluhisho nafuu kwa watu walio katika hatari.

Maendeleo ya kivinjari cha Mullvad itasaidia kuifanya Kivinjari cha Tor imara kwa sababu inaturuhusu kuendelea kushughulikia masuala ya urithi, kanuni na kurekebisha udhaifu.