Miaka miwili iliyopita tulianzisha mradi wa kuifanya VPN-kama programu tumizi ambayo inaunganisha mtandao wa Tor kwa watumiaji wa Android. Tunafamu kuwa tovuti nyingi na huduma inayowaunganisha watumiaji kupitia kivinjari katika kompyuta ya mezani huwa programu tumizi wakati inatumia mtandao katika simu. Ni muhimu kwetu sisi kushughulikia suala hili kwa watu wengi dunia kote tumia kifaa cha simy pekee kuunganisha kwenye internet, hasa kwa wale waliopo mataifa ya kusini na wenye hali ya hatari. Hutoa kivinjari kinachounganishwa kwenye mtandao na VPN inayoaminika katika mtandao wa Tor ni hatua muhimu katika kutoa njia mbadala zaidi kipindi linapokuja suala la vivinjari vya bure vinavyolenga faragha na kuinufaisha Tor Browser kipindi cha mbeleni wakati "VPN-yetu kama" programu tumizi inapozinduliwa.