Tofauti na vivinjari vingine katika soko, Mtindo wa biashara ya kivinjari cha Mullvad kuweka mtaji kwenye data ya tabia ya watumiaji. Mullvad hutengenza fedha zaidi kwa kuuza VPN yake, hawapo katika biashara ya kuuza data za watumiaji kutoka katika kivinjari.

Kivinjari cha Mullvad kilitengenezwa na Tor Project ambao wana rekodi iliyothibitishwa ya kujenga na kupeleka teknolojia huru na open-source ya kuhifadhi faragha kama vile Tor Browser, Onion Services, mtandao wa Tor n.k. ambazo zimewasaidia mamilioni ya watu kutoka katika jamii zilizo hatarini ambazo hutetea haki yao ya faragha na kutokujulikana mtandaoni.