Onion services huruhusu watu kuvinjari lakini pia kuchapisha kutokujulikana, ikiwemo kuchapisha tovuti zisizojulikana.

Onion services pia hutegemewa kwa mawasiliano ya data ya metadata na usambazaji wa faili, mwingiliano salama kati ya waandishi wa habari na vyanzo kama vile SecureDrop au OnionShare, kusasisha salama programu, na njia salama zaidi za kufikia tovuti maarufu kama Facebook.

Huduma hizi hutumia matumizi maalumu ya kiwango cha juu cha kikoa (TLD) .onion (badala ya .com, .net, .org n.k) na zinapatikana kwa njia ya mtandao wa Tor pekee.

Nembo ya Onion

Unapotumia tovuti inayotumia onion service, Tor Browseritaonyesha katika sehemu ya kuandika URL alama ya onion itaonyesha hali ya mawasiliano yako: salama na kutumia onion service.

Kujifunza zaidi kuhusu onion services, soma Jinsi Onion Service zinavyofanya kazi?