Tor imetekeleza sera za kutoka. Kila Tor relay ina sera ya kutoka ambayo inabainisha aina gani ya muunganiko wa nje unaruhusiwa au unakataliwa kutoka kwenye hiyo relay. Kwa njia hii kila relay inaamua huduma, mmiliki, na mtandao inaoutaka ili kuruhusu muunganiko, kulingana na uwezekano wa unyanyasaji na hali yake mwenyewe. Pia tuna timu iliyojitolea, Afya ya Mtandao, kuchunguza tabia mbaya ya rilei na kuwafukuza nje ya mtandao.

Ni muhimu kukumbuka kwamba ingawa tunaweza kukabiliana na aina fulani ya matumizi mabaya kama vile rilei mbaya katika mtandao wetu, hatuwezi kuona au kudhibiti kile ambacho watumiaji hufanya kwenye mtandao na hiyo ni kwa kubuni. Muundo huu kwa wingi unaruhusu matumizi ya manufaa kwa kuwapa wanaharakati wa haki za binadamu, wanahabari, waathirika wa unyanyasaji wa majumbani, watoa taarifa, maafisa wa kutekeleza sheria na wengine wengi faragha na kutokujulikana iwezekanavyo. Jifunze zaidi kuhusu watumiaji wetu na matukio ya manufaa ya Tor hapa.