Safi. Ikiwa unataka kutumia relays mbalimbali ili kutoa zaidi kwenye mtandao, tutafurahi kwa hili. Tafdhali lakini usiendeshe zaidi ya dazini chache katika mtandao ule, kwani sehemu ya lengo la mtandao wa Tor zimetawanyika na zina utofauti.

Ikiwa umeamua kuendesha relay zaidi ya moja, tafadhali pangilia "MyFamily" chagua sanidi katika torrc kwa kila relay, orodhesha relay zote (ikitenganisha na koma) ambazo ziko chini ya udhibiti wako:

MyFamily $fingerprint1,$fingerprint2,$fingerprint3

wakati kila fingerprint ni alama 40 bila nafasi kutambua fingerprint (bila kuweka nafasi).

Njia hiyo, Watumiaji wa Tor watajua namna ya kuepuka kutumia relay zako zaidi ya moja katika circuit moja. Unatakiwa kupangilia MyFamily kama una udhibiti wa kiuatawala katika kompyuta au mitandao yao, hata kama wote hawapo katika eneo moja kijografia.